Wednesday, January 9, 2013

MWANDISHI WA RADIO KWIZERA ISSA NGUMBA AKUTWA AMEUAWA PORINI

                                                      Marehemu Issa Ngumba
   MWANDISHI wa Habari wa kituo cha Radio Kwizera wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Issa        Ngumba (45) ameua kwa kunyongwa na kisha kupigwa risasi mkono wa kushoto huku simu zake mbili na Bastola iliyotumika kumshambulia ikiacha kando ya mwili wake porini.

Habari zilizopenyezwa kutoka wilayani Kakonko mkoani Kigoma na kuthibitishwa na kamanda wa Polisi wa mkoa huo Frasser Kashai, pamoja na Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Kigoma (KPC) Deo Sonkolo zimedai kuwa mwandishi huyo amekutwa ameuawa kwa kunyongwa shingo na watu ambao hawajajulikana.

Akizungumza na kwa njia ya simu, Sonkolo alisema kwamba mara baada ya kupata taarifa hizo aliwasiliana na waandishi habari wilaya ya Kibondo ambao waliwahi kufika eneo la tukio na kushuhudia uchunguzi wa Daktari Primus. 



Mwili wa marehemu umepatikana leo katika pori la Mlima Kajuluheta kijiji cha Muhange, wilayani humo majira ya asubuhi baada ya wananchi kufanya msako wa siku tatu tokea siku ua Jumapili ikiwa ni siku moja baada ya kutoonekana kwake.

Bastola iliyokutwa eneo la tukio imeokotwa ikiwa na risasi tano huku mifuko ya suruali ya marehemu ikiwa na noti moja ya Tsh10,000.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Frasser Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jeshi lake bado linangoja taarifa ya uchunguzi wa daktari sanjari na taarifa ya awali ya uchunguzi wa jeshi hilo toka eneo la tukio.

Sunday, November 11, 2012

KUTOKANA NA KUTOKUWEPO HEWANI KWA MUDA BLOG YAKO INAYOMILIKIWA NA RADIO YAKO YA NYUMBANI RADIO VICTORIA FM INAOMBA RADHI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA NAKWAMBA SASA INAAHIDI KUKUPA MATUKIO YOTE YA KILA SIKU PAMOJA NA HABARI

 Mkurugenzi Mkuu wa radio Victoria FM 90.6 na Mkurugenzi mkuu wa idara ya ufundi akirekebisha  mnala ulikuwa na tatizo katika antenner lililotokana na Mvua kubwa zilizonyesha hapo jana

Wakati akiendelea na matengenezo tulipata nafasi ya kupiga picha hii ikiwa ni moja kati ya majukumu yetu yakila siku kuhakikisha tunakupa taarifa juu matengenezo yanayoendelea kwaajili ya kukufahamisha pia

 Kwa mujibu wa mkurugenzi wa Radio Victoria fm Bw, Big boss Jan quaas kufikia majira ya saa 11 za jioni hii leo kila  kitu kitakuwa sawa, Uongozi wa Radio Victroia FM unaomba radhi kwa usumbufu kwani hatukuwa hewani kwa dakika kadhaa.